23 Apr 2024 / 67 views
Bayer Leverkusen wazidi kuweka rekodi

Josip Stanisic aliifungia Bayer Leverkusen bao la dakika za lala salama na kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa na sare ya 1-1 dhidi ya Borussia Dortmund.

Leverkusen walipata taji lao la kwanza la Ujerumani wakiwa wamebakisha mechi tano Jumapili iliyopita, na sasa wanalenga kuandikisha kampeni ya kwanza ya kutoshindwa katika Bundesliga.

Niclas Fullkrug aliwapa wenyeji Dortmund uongozi wa dakika ya 81 Jumapili.

Lakini Stanisic alifunga bao hilo katika dakika ya saba ya muda ulioongezwa na kufanya mechi 45 bila kufungwa katika mashindano yote.

Beki huyo wa Croatia, aliyetolewa kwa mkopo kutoka Bayern Munich, alifunga kwa kichwa akiunganisha kona ya Florian Wirtz hata baadaye kuliko wakati Jeremie Frimpong alipodumisha rekodi ya kutoshindwa msimu huu katikati ya wiki.

Kikosi cha Xabi Alonso kiliishinda West Ham kwa jumla ya mabao 3-1 katika robo-fainali ya Ligi ya Europa lakini ilihitaji bao la dakika ya 89 kutoka kwa Frimpong mnamo Alhamisi kuokoa sare ya 1-1 katika mkondo wa pili na kuendeleza mbio zao.

"Hatutaki tu kupoteza," Alonso aliiambia DAZN. "Bao lilikuwa la hisia sana, kusherehekea na mashabiki ilikuwa nzuri sana na ina maana kubwa kwetu sote. "Bado tunasubiri karamu yetu kubwa.

Sasa tutapona kidogo kisha tujiandae vyema kwa Stuttgart Jumamosi ijayo ambao utakuwa mchezo wa kusisimua sana."